Habari Mseto

Obado aachiliwa kwa dhamana ya mamilioni

August 28th, 2020 1 min read

NA JOSEPH WANGUI

Gavana wa Migori Okoth Obado anayeshtakiwa kwa ufisadi ameachiliwa kwa dhamana ya Sh8.7 milioni ama  pesa taslimu Sh2o milioni.

Jaji mkuu Lawrence Mugambi wa mahakama ya Milimani pia alitoa amri ya kumzuia Obado  kutika afisini mwake.

Afisa anayechunguza kesi yake aliagizwa kumsindikiza Obado akachukue bidhaa zake kutoka afisini mwake.

Korti hiyo pia ilimzuia Obado kusafiri nje ya Kenya. Gavana Obado na wanawe  ni washukiwa wa wizi ya mamilioni ya hela kutoka afisi za umma.

Alioshatakiwa nao waliachiliwa kwa dhamana ya kati ya Sh2 milioni na Sh8.2 milioni. Wote walizuiliwa kuingia afisi za kaunti.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA