Habari Mseto

Obado akana kuwapa sumu madiwani

July 1st, 2020 1 min read

IAN BYRON NA FAUSTINE NGILA
Gavana wa Kaunti ya Migori Okoth Obado na afisa wa barabara Moses Chamwada walitoa ushaidi wao kortini Alhamisi kuhusu madai kwamba waliwapa sumu wawakilishi wa wadi.

Kisa hicho kilijiri baada ya diwani wa Kanyamkago Kusini Graham Kagali kudai alipata matatizo baada ya kunywa chai kwenye hoteli ya Migori Machi.

Aliripoti kisa hicho kwa polisi huku akimwelekezea lawama gavana wa Migori Gavana Obado na afisa huyo.

Bw Obado na Bw Chamwada walimlaumu diwani huyo na Bw Duncan Owino kwa kushirikiana kumwaribia jina.

Gavana Obado alikana madai hayo mbele ya hakimu Dickson Onyango kwenye korti ya Migori Gavana Obado alitaja madai hayo kuwa ya uongo.

Maafisa wa upelelezi waliokuwa wakifanya uchunguzi walimkamata diwani huyo kwa madai hayo.

Alipokamatwa Bw Kagali alizuiliwa kwenye kituo cha polisi na akaachiliwa kwa dhamana ya polisi ya Sh 50,000.

Kesi hio itasikizwa tena Julai 14.