Obado na kakaye Ruto wakutana kukata miguu Raila eneo la Nyanza

Obado na kakaye Ruto wakutana kukata miguu Raila eneo la Nyanza

Na Justus Ochieng

GAVANA wa Migori Okoth Obado anapanga kubuni muungano na Naibu Rais William Ruto katika juhudi za kuyeyusha ushawishi wa kiongozi wa ODM Raila Odinga eneo la Nyanza.

Hayo yalijitokeza Jumapili gavana huyo alipomtembelea kakake Dkt Ruto, David Ruto, ambaye wandani wake wanamchukulia kama “mpanga mikakati ya kampeni za Dkt Ruto eneo la Nyanza”.

Wawili hao walikutana nyumbani kwa David mtaani Kileleshwa, Nairobi.

Mnamo Februari mwaka huu, kakaye Dkt Ruto alizindua vuguvugu la hasla mjini Kisumu na akaahidi kuzuru maeneo yote ya Nyanza kumnadi Naibu Rais.

Inaaminika kuwa mkutano kati yake na Gavana Obado Jumapili ni sehemu ya mikakati ya kumlemaza Bw Odinga katika ngome yake ya Nyanza. Mikakati sawa na hiyo inaendelezwa katika ngome za ODM Pwani na Magharibi ya Kenya.

Kambi ya Dkt Ruto inaaamini kuwa Bw Odinga ndiye mpinzani wake mkuu katika kinyang’anyiro cha urais 2022.

 

You can share this post!

Wachezaji wa mitaa ya Nakuru wapokea ufadhili kupiga jeki...

Pasta asherehekea kufariki kwa nabii TB Joshua, asema...