Kimataifa

Obama aungana na Biden katika kampeni kushawishi wapigakura

November 2nd, 2020 1 min read

Na MASHIRIKA

WASHINGTON DC, Amerika

ALIYEKUWA Rais wa Amerika, Barack Obama alijiunga na mgombeaji wa chama cha Democratic Joseph Biden kwenye kampeni za uchaguzi wa urais utakaofanyika Jumanne.

Katika wikendi ya mwisho ya kampeni, Biden na Obama walianza mikutano Jumamosi eneo la Flint kwa lengo la kushawishi idadi kubwa ya watu wajitokeze kupiga kura.

Baadaye, walifanya mkutano mwingine katika eneo la Detroit, ambapo msanii Stevie Wonder alitumbuiza umati.

Katika kampeni hizo, ilitangazwa kwamba Obama atafanya kampeni nyingine eneo la Atlanta na Florida Kaskazini mnamo Jumatatu.

Obama aliweza kuwashawishi wapigakura kutoka eneo la Michigan mara mbili, Kaunti ya Genesee na Flint.