Obiri atupia jicho mbio za mita 5000 baada ya kutamba Northern Ireland

Obiri atupia jicho mbio za mita 5000 baada ya kutamba Northern Ireland

Na GEOFFREY ANENE

BINGWA wa Mbio za Nyika za Dunia 2019 Hellen Obiri ametupia jicho mbio za uwanjani baada ya kuibuka mshindi wa mbio za nyika za Northern Ireland mita 8000 mwaka huu.

Mkenya huyo alitumia mbio hizo kma matayarisho ya kutetea mataji yake ya dunia nchini Amerika na Jumuiya ya Madola nchini Uingereza baadaye 2022 katika mbio za mita 5,000. Alinyakua taji Jumamosi kwa dakika 26:44 uwanjani Billy Neill Country Park.

“Kuna mashindano mengi 2022 yakiwemo ya dunia, Jumuiya ya Madola na Diamond League. Nitazungumza na meneja wangu na kocha nione ni yapi yatanifaa,” Obiri alisema.

Waingereza Hannah Irwin (27:04) na Mhairi Maclennan (27:21) walifunga tatu-bora.

Obiri ni Mkenya wa nne kushinda Northern Ireland baada ya Alice Aprot mwaka 2016, Caroline Chepkoech Kipkirui (2017) na Margaret Chelimo (2018). Makala haya yalivutia karibu wakimbiaji 600.

  • Tags

You can share this post!

AFCON: Wanane waaga dunia baada ya mkanyagano wa mashabiki...

Mvuvi afariki Lamu mawimbi makali yakiendelea kuyumbisha...

T L