Obiri na Korir kushindania ubingwa wa Ras Al Khaimah Half Marathon Milki za Kiarabu

Obiri na Korir kushindania ubingwa wa Ras Al Khaimah Half Marathon Milki za Kiarabu

Na GEOFFREY ANENE

WAKENYA Hellen Obiri, Judith Korir na Daniel Mateiko watarejea nchini Milki za Kiarabu kuwinda tuzo ya mshindi ya Ras Al-Khaimah Half Marathon ya Sh1.6 milioni hapo Februari 18.

Walikuwa katika makala yaliyopita na pia wametoa ithibati ya kushiriki mwezi ujao.

Obiri na Korir walikamata nafasi ya pili na nne mtawalia mjini Ras Al Khaimah mwaka 2022 ambapo pia waliandikisha muda wao bora katika kilomita 21 wa 1:04:22 na 1:05:28 mtawalia.

Obiri alishinda medali ya fedha ya mbio za mita 10,000 naye Korir nishani hiyo hiyo katika kilomita 42 kwenye Riadha za Dunia 2022 mjini Eugene, Amerika mtawalia.

Mateiko aliyekamilisha Ras Al Khaimah Half Marathon 2022 katika nafasi ya sita, ana muda bora wa dakika 58:26 kutoka nafasi ya tatu Valencia Half Marathon Trinidad Alfonso Zurich 2022.

Wakenya hao watatu walithibitisha kuwa watashiriki mbio hizo za kifahari ambazo mshindi atakayeweka pia rekodi mpya ya Ras Al Khaimah na dunia ataongezwa bonasi ya Sh608,899 na Sh12.4 milioni mtawalia.

Mara ya mwisho Mkenya alishinda mjini Ras Al Khaimah ilikuwa kupitia kwa Kibiwott Kandie (2020) na Fancy Chemutai (2018).

  • Tags

You can share this post!

Wengi wanufaika na mafunzo kutoka kwa shirika la Engage...

Wanafunzi 600 katika wadi ya Nairobi Kusini wapata basari

T L