Oboya Cup: Susa, Rongai zatua nusu fainali

Oboya Cup: Susa, Rongai zatua nusu fainali

Na JOHN KIMWERE

MATUMAINI ya Derby FC kutinga nusu fainali za kuwania taji la Patrick Oboya Cup yamegonga ukuta baada ya kuzabwa mabao 2-0 na Rongai FC kwenye robo fainali iliyopigiwa ugani Police Band, South B Nairobi.

Nayo South B United Sports Academy (SUSA) ilinyamazisha Mariakani Christian Centre (MCC) mabao 4-1 kupitia mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare bao 1-1. Rongai ilianza mchezo huo kwa kasi huku ikivamia lango la wapinzani wao kama nyuki na kucheka na wavu kunako dakika ya pili kupitia Glen Odhiambo.

Karibu ifunge bao la pili dakika mbili baadaye lakini Douglas Omwenga aligonga neti. Huku Derby ikisaka bao la kusawazisha ilifungwa bao la pili na kupoteza tumaini la kushinda mchezo huo. Bao hilo lilitupiwa wavuni na Douglas Omwenga.

”Hatuna lingine tumekubali yaishe bahati haikuwa yetu,” kocha mkuu wa Derby Ongeri Sam alisema na kupongeza vijana wake kwa kutinga mechi za hatua hiyo. Kwenye patashika ya pili bao la MCC lilitupiwa wavuni na Brian Olima kabla ya Shaban Chaka kusawazishia SUSA.

Kutokana na matokeo hayo, MUFYA itacheza na Team Ping Fc nayo SUSA itakutanishwa na Rongai FC. Team Ping FC ilijikatia tiketi ya nusu baada ya kusajili ushindi wa bao 1-0 mbele ya Cheza Sports.

Timu ya Derby FC iliyobanduliwa katika kipute cha kuwania taji la Patrick Oboya Cup…Picha/JOHN KIMWERE

You can share this post!

Red Carpet, Uthiru, WYSA zasonga mbele Tim Wanyonyi Super...

AC Milan wapoteza fursa ya kutua kileleni mwa jedwali la...

T L