Habari Mseto

Obure na Obodo wanaswa kwa mauaji

August 23rd, 2020 1 min read

NA VINCENT ACHUKA

Washukiwa wawili wamekamatwa Jumamosi kufuatia kifo cha mwanabiashara Kevin Omwenga.

Mfanyabiashara Chris Obure na Robert Obodo walikamatwa na maafisa  wa upelelezi wa DCI na wakapelekwa  kwenye kituo cha polisi cha Kilimani.

Duru za polisi zilisema kwamba Kevin Omwenga aliuwawa kutokana na mzozo  wa kibiashara kuhusiana na dhahabu.

Bunduki iliyotumika kumpiga risasi ilipatikana . Polisi walisema kwamba uchunguzi utafanyika kubaini kiini cha mfannyabiashara huyo kupigwa risasi.

TAFSIRI: FAUSTINE NGILA