Habari Mseto

Obure na Ouko kushtakiwa kwa mauaji

September 2nd, 2020 1 min read

Na Joseph Wangui

Wafanyabiashara wa Nairobi Chris Obure na Robert Ouko watashtakiwa kwa makosa ya mauaji ya Kelvin Omwenga yaliyotokea Kilimani mwezi uliopita.

Mkuu wa mashtaka aliambia korti ya Nairobi kwamba uchunguzi wa kubaini kilichosababisha kifo cha Bw Omwenga ulikuwa umekamilika,

Washukiwa hao waliomba kupewa dhamana. Korti inatarajiwa kufanya uamuzi Ijumaa Jioni.

Bw Omwenga wa aliyekuwa na miaka 28 alipigwa risasi nyumbani kwake Galana Suites Kilimani.

Uchunguzi ulionyesha kwamba Bw Ouko alimpiga risasi mwathiriwa baada ya kula chakula cha jioni wakiwa na marafiki zake na jamaa.

Bw Ouko alikuwa na mzungumzo na mwathiriwa chumbani kwake kabla ya mlio wa risasi kusikika. Bw Ouko baadaye alienda kuficha bunduki lake kwenye kampuni ya kibinafsi.

Tafsiri na Faustine Ngila