Habari Mseto

OCS afariki ajalini

August 26th, 2020 1 min read

By HILARY KIMUYU

Ajali mbaya iliyotokea Jumatano imesababisha kifo cha polisi mkuu baada ya gari lake la Toyota Belta kugogana na lori eneo la Ruiru Kamakis, Kaunti ya Kiambu.

Harrison Muteti Katecho, ambaye alikuwa OCS wa kituo cha polisi  cha Wanguru kaunti ya Kirinyanga ,kulingana na polisi gari lake ndogo lilipoteza mwelekeo na kugonga lori lilokuwa limeegeshwa kando ya barabara ili lilipe ushuru.

Kulingana  na polisi, Bw Muteti alipata maumivu ya kifuani na kichwani na kukibizwa hospitali ya Ruiru ambapo alitangazwa kuwa amefariki punde tu alipofikikishwa.

“Gari zote mbili zilikuwa zimeetoka pande ya Raui zikielekea barabara kuu ya Thika wakati dereva wa gari hiyo ndogo alipoteza mwelekeo kwa sababu zisizo julikana na  kugonga lori hilo,” ulisoma ujumbe wa polisi.

Lori hilo na gari hilo ndogo zilipelekwa  kwenye kituo cha polisi cha  Ruiru zikigoja uchuguzi huku mwili wa polisi huyi ukipelekwa  kwenye  chumba cha kuhifadhi maiti cha chuo  kikuu cha Kenyatta.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA