ODM yaomboleza

ODM yaomboleza

Na CHARLES WASONGA

MWENYEKITI wa ODM tawi la eneo bunge la Webuye Magharibi Ali Waziri amefariki.

Kulingana na ujumbe ulioweka na chama hicho Jumanne katika akaunti yake ya twitter, mwanasiasa huyo mkongwe alifariki Jumatano, Juni 7, 2021, jioni baada ya kuugua kwa muda mrefu.

“Tunaomboleza kifo cha mwanachama wetu wa kudumu na Mwenyekiti wa tawi letu la Webuye Magharibi Mheshimiwa Ali Waziri.

Bw Waziri ni mwanzilishi wa chama cha ODM. Kujitolea kwake katika kukivumisha chama chetu kilimfanya kuwa tegemeo letu katika eneo la Magharibi. Tutamkosa sana,” ODM ikasema kwenye ujumbe wake.

Kwa upande wale Katibu Mkuu wa chama hicho Edwin Sifuna pia alimwomboleza Bw Waziri akisema ODM imempoteza mlezi ambaye ambaye amekuza wengi kisiasa katika eneo la magharibi na Kenya kwa ujumla.

“Natuma rambirambi zangu kwa familia na marafiki wa rafiki yangu Ali Waziri aliyefariki Jumatano asubuhi. Mungu aiweke roho yake pema pema amani,” Katibu huyo mkuu akasema.

You can share this post!

Kuhalalisha au kutohalisha bangi kutahitaji sera mwafaka

Kilio cha wazee wa MauMau Kirinyaga