ODM yapokonywa ubunge Ganze ubingwa ukimwendea Kenneth Charo Tungule wa PAA

ODM yapokonywa ubunge Ganze ubingwa ukimwendea Kenneth Charo Tungule wa PAA

NA ALEX KALAMA

CHAMA cha Orange Democratic Movement (ODM) kimeshindwa kuhifadhi kiti cha ubunge Ganze, kaunti ya Kilifi baada ya mbunge wa eneo hilo Teddy Mwambire kushindwa na mpinzani wake wa chama cha Pamoja African Alliance (PAA) Kenneth Charo Tungule.

Mwambire ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti hiyo ya Kilifi aliibuka wa pili baada ya kupata kura 13,086 huku mgombea wa chama cha PAA aliyetangazwa kuwa mshindi wa kiti hicho akipata kura 41,719 naye Charo Samaki wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) akiwa nambari tatu kwa kura 4,117 huku naye Anderson Kenga wa chama cha Safina akivuta mkia baada ya kujizolea kura 917 pekee.

Mwambire ambaye alionekana kufanya miradi mingi ya maendeleo eneo hilo alirambishwa sakafu na ujio wa chama cha PAA eneo hilo ambacho kilionekana kubeba viti vingi vya uwakilishi wadi katika eneobunge hilo hasa ikizingatiwa kwamba mgombea wa kiti cha ugavana wa Kilifi kupitia chama cha PAA George Kithi anatoka eneo hilo.

MATOKEO YA UBUNGE GANZE

  MWANIAJI CHAMA KURA
1 KENNETH CHARO TUNGULE PAA 41,719
2 TEDDY MWAMBIRE ODM 13,086
3 CHARO SAMAKI UDA 4,117
4 ANDERSON KENGA AROSTE SAFINA 917

 

  • Tags

You can share this post!

KIKOLEZO: Penzi lakubali mabosslady!

Naibu Mwenyekiti wa ODM Kilifi apoteza kiti cha udiwani

T L