ODM yasema Raila amepona corona

ODM yasema Raila amepona corona

Na CHARLES WASONGA

KIONGOZI wa ODM sasa yuko salama baada ya vipimo vya hivi punde kubaini kuwa hana amepona Covid-19. Habari hizo zilifuchuliwa na chama hicho Jumatano kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.

“Tumefurahi kwamba Kiongozi wetu wa chama Raila Odinga amebainika kutokuwa na virusi vya corona. Tushukuru Mungu kwa hili. Mungu ambariki, Mungu aibariki Kenya.” ODM ikasema.

Bw Odinga aliugua mnamo Machi 10 na kulazwa katika Nairobi Hospital. Siku tatu baadaye alifichua kwamba alikuwa amepatikana na Covid-19.

Alijitenga nyumbani kwake Karen tangu wakati huo na amekuwa wakirejea Nairobi Hospital kwa ukaguzi wa kiafya kila mara.

Taarifa hiyo ya ODM ilitolewa baada ya Bw Odinga kufanya mkutano na viongozi wakuu wa chama hicho nyumbani kwake Karen, mkutano wa kwamba tangu alipougua.

Mkutano huo ulihudhuriwa na John Mbadi (mwenyekiti wa ODM), Junet Mohamed (kiranja wa wachache), Edwin Sifuna (Katibu Mkuu), Timothy Bosire (MwekaHazina) na mwenyekiti wa ODM Homa Bay Bw Glady Wanga. Pia alikuwepo kiongozi wa wachache katika seneti James Orengo ambaye pia ni seneta wa Siaya.

You can share this post!

Kamatakamata ya wasiovalia maski yafika mitaani

‘Nimeandaa mapishi 25 kutoka nchi mbalimbali Afrika...