Oguda amuonya Mwendwa dhidi ya safari za Harambee Stars

Oguda amuonya Mwendwa dhidi ya safari za Harambee Stars

Na JOHN ASHIHUNDU

Afisa Mkuu wa Kenya Premier League (KPL), Jack Oguda ameonya shirikisho la soka nchini, FKF kuhusu safari za ghafla za Harambee Stars.

Oguda alisema safari inayopangiwa timu hiyo kuzuru India, New Zealand, China na Taipei nchini Mumbai kati ya Juni 1 na 9 itaathiri ratiba ya mechi za KPL.

“FKF inafanya makosa kupangia timu ya taifa mechi ambazo hazifanyiki katika kalenda ya FIFA. Alisema ziara hiyo inayopangwa itavuruga ratiba ya timu za Zoo Kericho, AFC Leopards, Tusker, Ulinzi and Gor Mahia na Sony Sugar.

Oguda alisisitiza kwamba mechi za KPL zitaendelea kama ilivyopangwa, huku akimshutumu mkuu wa FKF, Nick Mwendwa kwa kuvuruga ratiba hiyo.

  • Tags

You can share this post!

Kamau kufika kortini baada ya wahandisi kukana kuiba...

Maraga: Najua Wakenya wamechoka lakini nina imani Uhuru...

adminleo