Menengai Oilers yafanya mabadiliko 9 ikivizia Homeboyz

Menengai Oilers yafanya mabadiliko 9 ikivizia Homeboyz

Na GEOFFREY ANENE

VIONGOZI Menengai Oilers wamefanyia kikosi kilichonyamazisha Kenya Harlequin wikendi iliyopita mabadiliko tisa tayari kuvaana na Homeboyz kwenye Ligi Kuu ya raga mjini Nakuru, kesho Jumamosi.

Kocha Gibson Weru, ambaye ametabiri mchuano huo utakuwa mgumu, amejumuisha Desterious Ifedha kujaza nafasi ya Emmanuel Mulla, Stanley Isogol ameingia mahali pa Kelvin Mulindo, naye Ibrahim Ayoo ataziba nafasi ya Kelvin Mukoyani.

Brian Sinei, Brian Ndirangu, Samson Onsomu, Steve Ochieng’, Austin Sikutwa na Eugene Lubanga watatumiwa katika nafasi za Wallace Onyango, Clinton Odhiambo, Tyson Maina, Kevin Mburu, Dennis Abukuse, Timothy Omela na Davis Nyaundi mtawalia.

“Tumewatumia Mulla, Mburu, Maina, Abukose na Mukoyani katika mechi tano mfululizo. Ni muhimu kuwapumzish kwa sababu ya mechi zijazo,” alisema Weru akifichua kuwa Lubanga atachezea Oilers kwa mara ya kwanza kabisa.

Aliongeza kuwa Derrick Mbaire aliumia mguu mazoezini naye Onyango anatibiwa goti.

“Ni mechi ngumu, lakini tumejiandaa vyema,” alisema. Homeboyz ni ya saba kwa alama 10.

Ratiba (Januari 15):

Topfry Nakuru vs Mwamba (RFUEA), Impala Saracens vs Blak Blad (Impala), Nondies vs KCB (Ngong Racecourse), Kenya Harlequin vs Strathmore Leos (RFUEA), Menengai Oilers vs Homeboyz (ASK Showground Nakuru), MMUST vs Kabras Sugar (Lurambi).

  • Tags

You can share this post!

Korti yazima hela za kaunti

KIKOLEZO: Grammys zimebaki stori tu!

T L