Okutoyi aporomoka tena kwenye viwango bora vya tenisi duniani

Okutoyi aporomoka tena kwenye viwango bora vya tenisi duniani

Na GEOFFREY ANENE

MKENYA Angella Okutoyi anaendelea kupoteza umaarufu kwenye viwango bora vya Shirikisho la Kimataifa la Tenisi (ITF).

Katika viwango bora vya tenisi ya chipukizi vilivyotangazwa mnamo Machi 29, Okutoyi alirushwa nafasi saba chini na kukalia nambari 150 duniani.

Inamaanisha kuwa Okutoyi, ambaye yuko katika kituo cha kukuza talanta cha Casablanca nchini Morocco, ameteremka jumla ya nafasi 23 tangu afikie nafasi yake ya juu kabisa katika viwango hivyo mnamo Februari 1 aliposhikilia nambari 127.

Alishinda mashindano mawili ya kimataifa ya chipukizi yaliyovutia zaidi ya mataifa 20 jijini Nairobi mwezi Januari na kupaa nafasi 59 kutoka 186.

Kuteremka kwake kwenye viwango hivyo ambavyo ni muhimu katika kuamua wachezaji wanaoshiriki mashindano ya kifahari ya Grand Slam, kutokana na kukosa kushiriki mashindano.

Alikuwa amepangiwa kuanza kushindana barani Ulaya kabla ya mwezi Mei, lakini mataifa mengi yameweka vikwazo vya kusafiri ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Anahitaji kuingia mduara wa wachezaji 100-bora ili aruhusiwe kushiriki mashindano ya Grand Slam. Alilenga kuanza kushiriki Grand Slam mwezi Mei nchini Ufaransa.

  • Tags

You can share this post!

Wakenya wakerwa na mbunge kuzindua televisheni

Afrika yalia Ulaya, hasa Ufaransa ‘inaiba’...