Michezo

Ole Gunnar amchemkia Sanchez

February 13th, 2019 1 min read

Na CECIL ODONGO

KOCHA wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amemchemkia mshambulizi Alexis Sanchez kutokana na fomu yake mbovu na kumwambia hawezi kumpanga kikosini asipoimarika kisoka

Sanchez aliaminiwa kuikoa Man U alipowajibishwa kutoka kwenye benchi wakati wa kichapo cha 2-0 mikononi mwa Paris Saint Germain(PSG) Jumanne Februarii 12,2019 lakini Imani hiyo iligeuka shuburi alipocheza kwa kiwango cha chini mno kuliko ilivyodhaniwa.

Mwanasoka huyo alichukua nafasi ya Jesse Lingard mwisho wa kipindi cha pili lakini akawa anapoteza mpira kirahisi na kukosa kulenga shuti lolote langoni mwa wapinzani wao kutoka Ujerumani.

“Siwezi kufanya chochote kuhusu Alexis Sanchez. Lazima atie bidii ili arejelee fomu yake ya zamani kwasababu tuna wachezaji wengine wazuri kikosini,” akasema Ole Gunnar ugani Old Trafford baada ya kupoteza mechi yake ya kwanza akiwaonoa Manchester United.

Mabao ya PSG yalimimimiwa wavuni na wachezaji Presnel Kimpembe na Kylian Mbappe katika kipindi cha pili kwenye mechi iliyomshuhudia nyota wa Man U Paul Pogba akilishwa kadi nyekundu na kuzamisha kabisa chombo cha mabingwa hao wa zamani wa EPL.

Hata hivyo, Ole Gunnar alisisitiza kwamba bado wana nafasi ya kuiadhibu PSG wakati wa mkondo wa pili wa mechi hiyo ya Klabu Bingwa Barani Afrika.

“Tutaenda mji wa Paris na kujituma kama kabisa. Ndiyo tuna mlima wa kuukwea lakini bado kila kitu hakijaenda mrama. Tutajaribu kupata bao katika kipindi cha kwanza na kama Man United tunaweza kufutilia mbali ushindi wao wa mkondo wa kwanza,” akasema Ole Gunnar.