Michezo

Olunga sasa aelekea Japan

August 8th, 2018 1 min read

NA CECIL ODONGO

MSHAMBULIZI wa Harambee Stars Michael Olunga anatarajiwa kujiunga na klabu ya Kashiwa Reysol ya Japan kutoka timu aliyokuwa akichezea soka, Guizhou Zhicheng ya Uchina.

Mchezaji huyo amekuwa nchini Uchina tangu mkataba wake wa mkopo na klabu ya Girona ya Uhispania utamatike. Girona hata hivyo wako tayari kumuuza Olunga baada ya kusajili idadi tosha ya wachezaji kutoka mataifa ya kigeni kulingana na sheria ya shirikisho la soka nchini Uhispania.

Baadhi ya klabu zilizokuwa zikimfuatilia fowadi huyo ni Real Sociedads  ya Uhispania lakini ripoti kutoka Japan zilithibitisha kwamba mwanadimba huyo atasajiliwa na timu ya Kashiwa Reysol.

Olunga alisakatia Thika United, Tusker na Gor Mahia katika ligi ya KPL kabla kuelekea Djurgaden IF ya Uswidi kuanizisha taaluma ya kucheza soka ya kulipwa.