Omar Shallo wa UDA akamatwa Mvita

Omar Shallo wa UDA akamatwa Mvita

NA FARHIYA HUSSEIN

MGOMBEA ubunge Mvita kwa tiketi ya United Democratic Alliance (UDA) Omar Shallo amekamatwa pamoja na mwaniaji udiwani Tudor Samir Bhalo na wakazuiliwa katika kituo cha polisi cha Makupa. 

Wawili hao walikuwa wakipinga kile walichodai kuwa ni maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kula njama na maajenti wa vyama vingine kuwakabidhi wafuasi wao karatasi zaidi ya moja kwa kila mpigakura kufanya udanganyifu.

Kulingana na wawili hao, kulitokea rabsha katika kituo kimoja ambapo maajenti wao walitimuliwa na wakati wakipinga udhalimu uliokuwa unaendelea, “polisi walitukamata sisi wadhulumiwa.”

  • Tags

You can share this post!

Hakuna kura ya ugavana Mombasa, Kakamega leo

Mbunge wa Mavoko asikitika mahakama kuzima CDF

T L