Omurwa ajiunga na Sektzia Ness Ziona FC ya Israel

Omurwa ajiunga na Sektzia Ness Ziona FC ya Israel

Na JOHN KIMWERE

BEKI wa Harambee Stars na Wazito FC, Johnston Omurwa amejiunga na klabu ya Sektzia Ness Ziona FC ambayo hushiriki Ligi Kuu nchini Israel.

Kando na kuchezea Wazito FC, mwanasoka huyo anajivunia kupigia klabu kadhaa za Ligi Kuu nchini ikiwamo Mathare United na AFC Leopards maarufu Ingwe.

”Ni kama ndoto kwa mchezaji wa Harambee Stars kupata nafasi kushiriki soka la kulipwa hasa wakati Kenya imefungiwa na Shirikisho la Soka la Duniani (FIFA),” alisema.

Omurwa alikuwa kati ya wachezaji walioshiriki mchezo mechi ya kuwania tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Afrika (AFCON) dhidi ya Misri 2020.

Itakumbukwa mwaka 2021 ingawa hakufaulu alishiriki majaribio kujiunga na klabu ya Bidvest Vits FC ya Afrika Kusini.

Kwingineko, Masoud Juma anayeshiriki soka ya kulipwa nchini Morocco wikendi aliibuka nyota alipofunga bao la pekee na kusaidia klabu yake kutia kapuni alama tatu muhimu kwenye kampeni za ligi ya Botola.

Mkenya huyo ambaye husakatia Difaa Hassan El-Jadida alifunga bao hilo walipokutanishwa na Rapide Qued Zem.

Baada ya matokeo hayo, Difaa Hassan El-Jadida inafunga nane bora kwa kutia kapuni alama 38 kutokana na mechi 30. Nayo WYDAD Casablanca inaongoza kwa kuzoa alama 63, tatu mbele ya Raja Club Athletic.

  • Tags

You can share this post!

Wakazi wa Kiambu wahimizwa wakumbatie kilimo

Khalwale, Echesa waahidi kupiga jeki azma ya Malala

T L