Habari Mseto

Omwenga azikwa

August 27th, 2020 1 min read

NA Ruth Mbula

 

Aliyekuwa mwanabiashara wa Nairobi Kevin Omwenga alizikwa Jumamosi wiki moja baada ya kupigwa risasi nyumbani kwake Galana Suites Kilimani kesi ambayo bado inaendelea kuchunguzwa.

Mwanabiashara huyo alizikwa kijiji cha Soko, Kitutu Chache Kusini kaunti ya Kisii sherehe ambayo ilihudhuriwa na wanabiashara na wanasiasa.

M Steve Mbogo, Zaheer Jhanda, Don Bosco na Charles Nyagoto ni kati ya madiwani waliohudhuria mazishi hayo.

Wanasiasa walisema kwamba Bw Omwenga alikuwa mkakamavuna kifo chake ni cha kujutiwa.

Bw Nyagoto (Bogeka, Kisii) alisema kwamba walikuwa wakifuatilia uchunguzi alisema kwamba wanafuat.ilia uchunguzi huo na wanatarajia haki itatendeka. “Hatutarajii kitu ingine isipokua haki.”

Marafikii na jamaa waliomba haki iteendeke.

Dunguye Wycliffe alisema kwamba wote ni mayatima kwani mamayao na nduguye wa kike walifariki mwaka jana.

“Haki ittendeke kwa dungu yangu.Nilimlea Kevin baada ya kifo cha babayangu.Aliyekupiga risasi anajua ni kwanini alifanya hivo.Mungu atafanya kama yeye,” alisema.

“Familia yetu inataka maombi kwani Kevin alifariki siku yenye mama yangu alifariki,”alisema.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA