Ondoa chunusi usoni kwa kutumia maji ya mshubiri(Aloe vera).

Ondoa chunusi usoni kwa kutumia maji ya mshubiri(Aloe vera).

Na WINNIE ONYANDO

Je, uso wako umejaa chunusi? Usihofu kwa kuwa maji au juisi ya mshubiri ni tiba.

Kulingana na ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni(WHO), asilimia 90 ya watu kwa hali moja au nyingine maishani wamekumbwa na tatizo la chunusi wanapokua. Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa asilimia 80 ya watu walio kati ya miaka 15 na 30 hukumbwa na tatizo hilo ulimwenguni.

Chunusi sio tu shida miongoni mwa wanawake bali pia wanaume. Mtu anapojitazama kwenye kioo na kupata amefura fura usoni, anakosa kujiamini miongoni mwa wenzake.

Chunusi husababishwa na aina ya vyakula tunavyokula, mabadiliko ya homoni, aina ya mafuta tunayotumia usoni au hata kurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.Japo huu ni ugonjwa wa ngozi, matumizi ya maji au juisi ya mshubiri huweza kuondoa na kutibu chunusi usoni au hata mwilini ikiwa utaratibu ufaao umefuatwa.

Utaratibu

v Nunua mshubiri mbichi dukani.

v Osha mshubiri yako kwa kutumia maji safi

v Toa miiba kwenye kila upande wa mshubiri kwa kutumia kisu

v Katakata mshubiri katika vipande vidogo vidogo kisha uchanganye kwenye blenda. Ikiwa huna blenda, gawa mshubiri katikati, kisha ukame ili kutoa juisi au maji yake kwenye bakuli safi

v Baada ya kupata juisi ya mshubiri, paka kwenye uso au sehemu ya ngozi iliyoathiriwa. Kaa kwa muda wa dakika thelathini kisha uoshe kwa kutumia maji vuguvugu.

Rudia utaratibu huo kila siku ili upate matokeo bora.

  • Tags

You can share this post!

Afrika isilalamikie Ulayakuipa lakabu ‘bara la giza’

Habari ndio hiyo!