Habari Mseto

Onyo kwa wanaosafirisha mafuta chafu

March 20th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Tume ya Kudhibiti Kawi nchini (ERC) imetoa onyo kali kwa wasafirishaji wa mafuta ya gari katika hatua ya kudhibiti uchafuaji wa mafuta.

ERC imetishia kubatilisha leseni za wauazaji wote wa mafuta ambao gari magari yao yatapatikana yakiwa yamepakiwa katika maeneo au vituo vya mafuta visivyo na leseni au kusafirisha mafuta yaliyo na uchafu.

Madereva watakaopatikana wakiendesha magari ya kubeba mafuta kwa njia isiyofaa au kuegesha magari hayo katika maeneo yasiyofaa watafungiwa kuendesha malori ya kubeba mafuta na gesi ya petrol.

Mwaka 2017 Aprili, Waziri wa Kawi Charles Keter alitaja Kisumu, Eldoret na Nakuru kama maeneo ambayo ‘biashara chafu’ za mafuta hufanyiwa.

Kulingana na waziri huyo, ikiwa mswada wa mafuta utapitishwa Bungeni, baadhi ya changamoto kama hizo zitatatuliwa.