Oparanya apanga kuachia serikali kuu ujenzi wa hospitali ya rufaa

Oparanya apanga kuachia serikali kuu ujenzi wa hospitali ya rufaa

Na BENSON AMADALA

SERIKALI ya Kaunti ya Kakamega inapanga kukabidhi Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kakamega kwa serikali kuu, ili ikamilishe ujenzi wake ambao kwa ujumla unatarajiwa kugharimu Sh6 bilioni.

Gavana Wycliffe Oparanya, amesema waliafikia uamuzi huo kutokana na changamoto za kifedha ambazo zimekabili kaunti hiyo katika kukamilisha ujenzi huo.

Alisema kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi huo ambao unagharimu Sh2.5 bilioni inaendelea na karibu ujenzi unakamilika.

Hospitali hiyo inatarajiwa kutoa huduma spesheli za kimatibabu kwa wakazi wa Nyanza, Magharibi na wale wanaotoka sehemu ya Bonde la Ufa.

Ujenzi wa hospitali hiyo ulikwama baada ya mkandarasi aliyekuwa akiutekeleza kujiondoa, akidai alipwe deni la Sh280 milioni.

You can share this post!

TAHARIRI: Tutahadhari sana na aina hii mpya ya corona

Mwandani wa Ruto ‘asaliti’ vijana

T L