Habari Mseto

Othuol Othuol kuzikwa Oktoba 24

October 13th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Mcheshi wa Churchill Show Ben Maurice amaafuru Othuol Othuol aliyefariki Jumapili baada ya kugonjeka uvimbe wa ubongo atazikwa Oktoba 24.

Kwenye ujumbe uliotolewa na  wacheshi wenzake kwa mwenyekiti Ken Waudo, mazishi hayo yanatarajiwa kugharimu milioni moja.

“Mipango ya kusadirisha mwili wake nyumbani kwao Ndere, Alego kaunti ya Siaya inayopangwa kufanyika 25 Oktoba mazishi yake yatagharimu Sh700,00 hadi Sh1 milioni,” alisema.

Alisema kwamba mwili wa mcheshi huyo ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha Chiromo.

Wacheshi, familia na marafiki wanafika Kitengela na hotelini Nairobi kwa mipango ya mazishi na kutoa risala za rambi rambi.

Alisema kwamba kutakuwa na harambee ya kuchanga pesa za mazishi. Othuol alifariki Okotoba 11, 2020 lipokuwa akitibiwa kwenye hospitali ya Kenyatta wiki mbili zilizopita.

Alipatikana na ugonjwa wa TB miezi kumi iliyopita na kulazwa Kenyatta. Alifariki akiwa na miaka 31. Mwezi Juni alizimia nyumbani kwake  na kukibizwa  hospitali ya Kitengela ambapo alitibiwa na kurusiwa kwenda nyumbani ,alilazwa tena mara ya mbili zilizopita na kufariki Jumapili.