Otieno afungia AIK bao kuibuka mchezaji bora wa mechi Uswidi

Otieno afungia AIK bao kuibuka mchezaji bora wa mechi Uswidi

Na GEOFFREY ANENE

BEKI Eric Otieno alitawazwa mwanasoka bora wa mechi baada ya timu yake ya AIK kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya wageni Sirius kwenye Ligi Kuu ya Uswidi, Jumamosi usiku.

Christian Kouakou na Patrik Karlsson Lagemyr walitetemesha nyavu za AIK dakika ya 22 na 39 mtawalia.

Jordan Larsson alipunguza mwanya hadi 2-1 dakika ya 43 huku Otieno akisawazisha 2-2 kabla ya mapumziko mbele ya mashabiki 25, 619. Matokeo hayo yaliwezesha AIK kudumisha rekodi ya kutoshindwa na Sirius hadi mechi 14.

AIK, ambayo imeajiri mshambulizi Henry ‘Meja’ Atola na kiungo Collins Sichenje kutoka Kenya, inaongoza ligi hiyo ya klabu 16 kwa alama 20 baada ya kujibwaga uwanjani mara 10.

Iko pointi tatu mbele ya Hammarby na Hacken zinazofuatana katika nafasi ya pili na tatu mtawalia baada ya kusakata michuano minane kila mmoja. Meja alikuwa katika kikosi cha siku ya mechi, lakini hakutumiwa. Sichenje hakujumuishwa katika kikosi cha siku ya mechi.

  • Tags

You can share this post!

Huhitaji hela nyingi kununua chakula muhimu kwa afya yako

Re-Union FC yaweka mikakati kurejesha fahari kama zamani

T L