Habari Mseto

Outering haijapunguza msongamano licha ya kupanuliwa

February 7th, 2019 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Serikali itapanua zaidi barabara ya Outering kunganisha na Thika Super Highway kwa lengo la kudhibiti msongamano wa trafiki katika barabara hiyo.

Mamlaka ya Barabara za Miji (KURA) itatengeneza njia zaidi katika barabara hiyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa lengo la barabara hiyo limetimizwa.

Barabara hiyo imeanzia eneo la Eastlands, moja ya maeneo yaliyo na watu wengi zaidi Nairobi na utengenezaji wake ulilenga kupunguza msongamano.

Hata hivyo, bado msongamano mkubwa ushuhudiwa karibu kila siku hasa eneo ambako barabara hiyo inaungana na Thika Super Highway hasa wakati wa shughuli nyingi.

Barabara hiyo ilifunguliwa upya zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Tayari, njia ya kati katika barabara hiyo eneo la umoja inaendelea kutengenezwa.

Disaini ya barabara mpya imekamilika na itaanza kujengwa hivi karibuni kulingana na afisa wa mawasiliano wa KURA Bw John Cheboi.