Owino: Hatuendi kutalii Ghana bali kushindana

Owino: Hatuendi kutalii Ghana bali kushindana

Na JOHN KIMWERE

TIMU za taifa wanaume na wanawake za voliboli ya ufukweni ziliondoka leo asubuhi kuelekea jijini Accra, Ghana kushiriki mechi za kuwania tiketi ya Michezo ya Jumuiya ya Madola.

Shindano hilo litafanyika Machi 24 hadi 29. Timu za wanawake zitakosa huduma za wachezaji wawili, Phosca Kasisi na Yvonne Wavinya walioshiriki Michezo ya Olimpiki nchini Japan mwaka jana.

Wawili hao walitemwa baada ya mchezo wao kudidimia. ”Kama nilivyoahidi hatuendi kutalii nchini Ghana bali nia yetu itakuwa kushinda tiketi ya kuwakilisha bara la Afrika,” kocha wa timu za wanaume, Patrick Owino alisema na kuongeza hata hivyo wanafahamu haitakuwa mteremko lazima wajitume.

Meneja wa vikosi hivyo, Sammy Mulinge anashikilia kuwa ana imani wachezaji hao wamekaa vizuri kukabili wapinzani wao. ”Tunaamini tumeshiriki mazoezi ya kutosha na wachezaji wapo fiti pia tayari kushiriki ngarambe hiyo,” alisema.

Kipute hicho kitashirikisha Nigeria, Msumbiji, Gambia na wenyeji Ghana. Timu za wanaume zinajumuisha: Nicholas Lagat, Donald Mchete, Ibrahim Odour na James Mwaniki huku wanawake wakiwa: Veronica Adhiambo, Naomi Too, Brackcides Agala na Gaudencia Makokha. Wengine katika ujumbe huo ni;Salome Wanjala (kocha wa timu za wanawake), Sammy Mulinge(meneja), Mzinga Kyalo (refarii) na daktari Sarah Karongo.

You can share this post!

Bodaboda walia polisi jijini bado wanawadhulumu

MUME KIGONGO: Kunenepa matiti ni kawaida lakini kunaweza...

T L