Bambika

Pacha Mtumishi na Mchungaji watemana, sababu hii hapa

February 7th, 2024 1 min read

NA SINDA MATIKO

MCHEKESHAJI Mtumishi amekanusha tetesi za kuwa bifu ndio iliangamiza ushirikiano wake na pacha wake wa vichekesho Mchungaji.

Mtumishi na Mchungaji ni kati ya vipaji vya vichekesho vilivyoibuliwa na Churchil Show na kuishia kuwa brandi kubwa.

Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni wachekeshaji hao hawajakuwa wakishirikiana kwenye sanaa yao kama zamani na kupelekea kuzuka kwa tetesi kwamba wametibuana.

“Kikweli bado tupo vizuri sema ni maisha ndio yametokea. Maisha yanapotokea kila mtu huwa na njia yake. Kasi yake sio yangu na kasi yangu sio yake ndio sababu hatupo pamoja kikazi kama zamani. Lakini ikitokea kazi na ikahitajika tuwe sote basi tunapatikana,” Mtumishi anasema.

Kwa maana hiyo Mtumishi kamaliza ukakasi kwamba mahusiano yao hayapo.