Habari Mseto

Padre aliyehatarisha maisha ya watu ashtakiwa baada ya kupona

April 17th, 2020 2 min read

Na Richard Munguti.

Padre wa kanisa la Katoliki Richard Onyango Owuor yuko motoni kwa kuamnukiza wananchi maradhi ya Corona tangu aliporejea nchini kutoka jijini Roma katikati mwa Machi mwaka huu.

Padre Owuor anayeendelea na masomo ya upadri jijini Roma alifikishwa katika mahakama ya Milimani ya Milimani baada ya kuruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospitali ya Mbagathi.

Kasisi huyo alitiwa nguvuni baada ya kukamilisha ibada ya mazishi eneo la Magharibi.

Alilazwa katika hospitali ya Mbagathi baada ya kupatikana na ugonjwa wa Corona ambao umesababisha vifo vya wattu zaidi 100000 ulimwennguni.

Madaktari wa Serikali waliomuhudumia walisema amepona.

Alipofikishwa mbele ya hakimu mwandamizi Martha Nanzushi Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma DPP kupitia kwa kiongozi wa mashtaka Bw Abel Amareba aliomba mahakama iamuru Kasisi Owuor azuiliwe kwa siku tano.

“Naomba hii mahakama iamuru mshukiwa azuiliwe kwa siku tano katika korokoro ya polisi ili wachunguzi wakamilishe kuwahoji mashahidi,” Amareba.

Amareba alisema kasisi alitangamana na wananchi wengi pamoja na mapadri wa Kanisa Katoliki akitoa huduma pamoja na kuongoza ibada ya mazishi.

“Polisi hawajapokea taarifa kutoka kwa watu aliotangamana nao,” mahakama ilijulishwa.

Aliongeza kusema ugonjwa wa corona ni janga la kimataifa na wananchi wanauchukua kuwa tisho na “hata wananchi wengine wameshambulia watuhumiwa wanaoeneza maradhi haya hatari na kupelekea kuuawa kwa mshukiwa mmoja.”

Amareba alisema kasisi yuko na ushawishi mkubwa na atawavuruga mashahidi.

Lakini mawakili John Were, Francis Wasuna na Andrew Okumu walipinga vikali ombi la DPP kwamba mshukiwa azuiluwe siku tano.

“Haikufaa polisi wamshike Kasisi kabla ya kukamilisha uchunguzi,” akasema Bw Were.

Wasuna alisema hakuna shtaka alililofunguliwa kasisi kwa vile mashahidi hawajaandikisha ushahidi utakaowaslishwa kortini.

“Hakuna mashahidi walioandikisha ushahidi kwa vile itabidi waende hospitali kupimwa na ithinitishwe ni Kasisi Owuor aliwaambukiza,” alisema Wasuna.

Mawakili wanaomwakilisha Padre Owuor washauriana baada ya agizo azuiliwe siku mbili korokoro ya polisi. Picha/ Richard Munguti

Hakimu alifahamishwa endapo kasisi atapatikana na hatia atatozwa faini ya Sh30000.

Mawakili walisema.shtaka atakayoshtakiwa kasisi sio mbaya na kumsihi hakimu aamuru mshukiwa awe huru kwa vile ” ilikuwa aanze masomo kwa mtandao kuroka Roma.”

Mawakili walisema usafiri wa ndege umesitishwa na “kamwe mshtakiwa hawezi akatoroka na pia hajui mashahidi watakaofika kortini watatoka wapi.”

Akitoa uamuzi hakinu alisema kesi ya kasisi huyo iko na umuhimu mkubwa kwa umna.

“Nakubaliana na upande wa mashtaka kesi hii iko na umuhimu mkubwa kwa umma ikitiliwa maanani wananchi wengi wameambuikizwa na watu wanaitoka ng’ambo,’Hakimu.

Alipunguza siku DPP alizoomba tano kwa siku tatu.