Kimataifa

Pakistan yawalipa wakulima wanaokamata nzige na kuunda chakula

June 12th, 2020 1 min read

NA AFP

Nchi ya Pakistan imekuwa ikikamata nzige na kutengeneza chakula cha kuku kama njia mojawapo ya kupambana na uvamizi wa wadudu hao ambao wameharibu mimea nchini humo na uzalishaji chakula.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo Imra Khan ameweka mikakati ya kuendeleza mradi huo katika jimbo la Breast-Basket Punjab ambapo wanakijiji wanalipwa kukamata nzige hao ambao baadaye hukaushwa, kukatakatwa na kutumika kama chakula cha kuku.

Wakulima wa nchi hiyo wanasumbuliwa na nzige hao huku mapato yao yakishuka mno.

Alichagua wilaya hiyo ya Punjab kwa sabau hawakua wametumia dawa ya kuua wadudu hao na hivyo nzige hao hawawezi kuleta mathara yeyote yakitumiwa kama mlo wa kuku.

Muhammad Khurshid na Johar Ali kutoka Wizara ya Lishe waliwahimiza wananchi kutumia nzige hao kama chakula kwasababu wana protini zinazohitajika mwilini.

“Kwanza tulisoma alafu tukawafunza wananchi jinsi ya kuteka nzige hao kwa neti,”alisema Khurshid.

Nyakati za usiku nzige hao huwa rahisi kuwateka kwa sababu hukusanyika mahali pamoja kupumzika.

Kwa malipo ya Rupia 20 kwa kilo moja, wakazi wamekuwa wakijikaza kuwateka usiku mzima.

Mkulima mmoja aliyepoteza mimea yake yote kwa nzige alisema kwamba yeye na mwanawe walilipwa Rupia 1600 kwa kuwateka nzige hao siku moja.