Palmeiras wazamisha Flamengo na kutwaa taji la tatu la Copa Libertadores

Palmeiras wazamisha Flamengo na kutwaa taji la tatu la Copa Libertadores

Na MASHIRIKA

PALMEIRAS walipepeta Flamengo ambao ni washindani wao katika Ligi Kuu ya Brazil 2-1 uwanjani Centenario, Uruguay, mnamo Jumamosi na kutia kapuni ubingwa wa Copa Libertadores.

Deyverson aliyetokea benchi katika kipindi cha pili alichuma nafuu kutokana na masihara ya Andreas Pereira na kufungia Palmeiras bao la ushindi katika dakika ya tano ya muda wa ziada. Gabriel Barbosa alikuwa amesawazishia mabingwa wa 2019 Flamengo jijini Montevideo – mahali ambapo fainali ya kwanza ya Kombe la Dunia iliandaliwa.

Goli hilo la Barbosa lilipatikana baada ya Raphael Veiga kuwafunguliwa Palmeiras ukurasa wa mabao. Palmeiras sasa wameshinda taji la Copa Libertadores mara tatu.

You can share this post!

JAMVI: Bado sijaanza kampeni za 2022 – Ruto

Depay na Coutinho wabeba Barcelona dhidi ya Villarreal...

T L