Papa Francis aanza ziara yake rasmi Afrika

Papa Francis aanza ziara yake rasmi Afrika

Na MASHIRIKA

KINSHASA, DRC

PAPA Francis ameanza rasmi ziara yake ya siku sita katika nchi za Afrika.

Kiongozi huyo wa Kanisa la Katoliki amezuru nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo leo Jumatano kama njia ya kuombea amani katika nchi hiyo inayokumbwa na mzozo.

Kanisa Katoliki jijini Kinshasa lilisema kwamba ziara hiyo inalenga maombi maalum ya amani.

Hii ni safari yake ya 40 nje ya nchi tangu alipotawazwa kuwa papa.

Anatarajiwa kukaa katika nchi hiyo hadi Februari 3, atakapoondoka kuelekea Juba na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby.

  • Tags

You can share this post!

Familia zaidi ya 1,000 zilizoathirika na moto kusubiri...

MCAs wa UDA Nairobi wataka viongozi wao wawili waadhibiwe...

T L