PATA USHAURI WA DKT FLO: Vidonda kwenye ulimi balaa beluwa, nifanyeje?

PATA USHAURI WA DKT FLO: Vidonda kwenye ulimi balaa beluwa, nifanyeje?

Mpendwa Daktari,

Nitakabiliana vipi na vidonda kwenye ulimi wangu?

Farida, Mombasa

Mpendwa Farida,

Huenda vidonda ulivyo navyo kwenye ulimi ni kutokana na vidonda vya homa ambavyo husababishwa na virusi vya Herpes simplex. Watu wengi huambukizwa virusi hivi utotoni na kujificha mwilini, kabla ya kuchipuka tena ukiwa na msongo wa mawazo, ukiwa na mafua au kukiwa na mabadiliko ya kihomoni mwilini. Huenda vidonda vya kila mara vikasababishwa na maambukizi ya ukuvu. Vyaweza tibiwa kwa kutumia matone au krimu za kukabiliana na ukuvu.

Huenda pia unapata vidonda vinavyofahamika kama aphthous ulcers, kwa jina lingine canker sores. Wakati mwingi hakuna kinachosababisha vidonda hivi. Huenda vikatokea ukijiuma, ukiwa na msongo wa mawazo; usipolala vyema; ukiwa na kinga mwili dhaifu kama wakati unapougua mafua; kukiwa na mabadiliko ya kihomoni; ukiwa na maambukizi ya bakteria ukuvu au virusi.

Kuna baadhi hupata hali hii kutokana na sababu za kijenetiki, na hii huenda ikatokana na maradhi ya auto-immune disease. Haya ni maradhi ambapo mfumo wa kinga mwilini huunda kingamwili (antibodies) dhidi ya baadhi ya tishu mwilini mwako dhidi ya safu za kamasi. Pia litakuwa jambo la busara iwapo utafanyiwa uchunguzi wa utapia mlo wa virutubisho vya vitamini B12 na folate, vile vile maradhi ya Behcet’s, crohn’s disease na lupus.

Ili kudhibiti vidonda hivi, gogomoa ukitumia maji ya chumvi au dawa maalum ya mdomo, tumia krimu ili kukabili maumivu na uvimbe, na pia tumia dawa za kukabiliana na virusi na vidonda vya mafua. Epuka vyakula moto, vilivyo na chumvi kali, vilivyo na viungo vingi au vilivyo na asidi nyingi. Kunywa maji kwa wingi na udumishe afya ya mdomoni. Pia utanufaika kutokana na vijalizo vya virutubisho vya vitamini B na folic acid. Ikiwa vidonda hivi vitaendelea kwa zaidi ya wiki mbili, utahitaji kukaguliwa na datkari.

You can share this post!

SHINA LA UHAI: Hofu ya makali ya virusi vipya vya corona

Olunga afunga hat-trick akisaidia Al Duhail kukung’uta Al...