Michezo

Paul Put ajiuzulu Harambee Stars, Okumbi achukua nafasi yake kwa muda

February 19th, 2018 1 min read

Bw Paul Put akihutubia wanahabari awali. Alijiuzulu Februari 19, 2018 kama kocha mkuu wa Harambee Stars. Picha/ Maktaba

Na JOHN ASHIHUNDU

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Harambee Stars, Paul Put amejiuzulu Jumatatu alasiri akidai kukumbwa na shughuli nyingi za kibinafsi.

Bw Put amejiuzulu wakati ambapo timu hiyo inajiandaa kwa mechi za kufuzu kwa fainali za 2019 AFCON.

Mara tu alipopeana barua ya kujiuzulu, Shirikisho la Soka (FKF) limeanza kutafuta mtu wa kujaza nafasi hiyo, ambayo itashikiliwa kwa muda na naibu wake, Stanley Okumbi.

Katika ujumbe mfupi uliotumwa kwa vyombo vya habari, FKF imempongeza kocha huyo kwa huduma zake alipokuwa mamlakani huku ikimtakia kila la heri kokote aendako.