Pedro atema mkewe na kuchumbia kahaba

Pedro atema mkewe na kuchumbia kahaba

Na CHRIS ADUNGO

NYOTA wa Chelsea, Pedro Rodriguez, 32, amejinasia penzi la mrembo mpya mzawa wa Uhispania miezi michache baada ya kutemana rasmi na aliyekuwa mkewe Carolina Martin.

Sogora huyo anayehemewa sana na Man-United, alionekana akiponda raha na kidosho huyo anayekisiwa kuwa mmoja wa makahaba wageni katika mkahawa mmoja maarufu jijini Barcelona.

Baada ya kushiriki ulevi nyumbani kwa Pedro, wawili hao walipigwa picha za pamoja zilizopakiwa baadaye na mwanasoka huyo wa zamani wa wa Barcelona kwenye mtandao wake wa Instagram.

Katika mojawapo ya picha hizo, Pedro alikuwa amevua shati huku akisakata densi na barafu ya moyo wake sebuleni.

Kilichoashiria ukubwa wa kiwango cha kukomaa kwa penzi lao ni picha zilizomuonyesha Pedro akiyapapasa maziwa ya kichuna huyo aliyekuwa akimpiga mabusu mazito, kumshika kiuno na kukichezea kidevu chake wakati wote wa kujistarehesha kwao.

Hadi alipokatiza uhusiano wake na Carolina mwishoni mwa mwaka jana, Rodriguez alikuwa amejaliwa mtoto mmoja wa kiume kwa jina Bryan. Wawili hao walianza kutoka kimapenzi mnamo 2009 kabla ya kula yamini ya ndoa mnamo Juni 2015 katika sherehe ya harusi iliyohudhuriwa na wanasoka wengi maarufu wa Barcelona wakati huo.

Carolina ambaye ni mhasibu kitaaluma, ni rafiki mkubwa wa kipusa Daniella Semann ambaye ni mke wa kiungo matata Cesc Fabregas aliyewahi kucheza pamoja na Rodriguez kambini mwa Barcelona.

Carolina na Daniella walianza kupalilia urafiki wao mnamo 2014 baada ya kuwa miongoni mwa mashabiki ambao wasingekosa kabisa kuhudhuria mchuano wowote wa Barcelona kwa minajili ya kushabikia vidume vyao.

Mkataba kati ya Pedro na Chelsea unatamatika rasmi mwishoni mwa msimu huu, jambo ambalo huenda likamchochea kutua ugani Old Trafford kuvalia jezi za Man-United chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer. Ingawa hivyo, gazeti la The Sun linashikilia kwamba fowadi huyo atakuwa mwepesi wa kurejea Uhispania na kutulia katika ndoa na mpenzi wake mpya huku akivalia jezi za Real Betis, Sevilla au Villarreal ambao wamefichua azma ya kujitwalia maarifa yake mwishoni mwa msimu.

Pedro aliwahi pia kutikisa buyu la asali na mshindi wa zamani wa taji la Miss Bumbum nchini Brazil, Ellen Santana.

You can share this post!

Umoja yasajili wanavikapu 3

Real yaitaka Arsenal kuamua kuhusu hatima ya Auba

adminleo