Pendekezo barabara ya jiji la Nairobi ipewe jina la Raila

Pendekezo barabara ya jiji la Nairobi ipewe jina la Raila

Na COLLINS OMULO

KIONGOZI wa Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga huenda akawa kiongozi mpya kupata barabara inayoitwa kwa jina lake jijini Nairobi.

Hii ni iwapo madiwani wa Bunge la Kaunti ya Nairobi watapitisha mswada unaounga mkono hatua hiyo uliodhaminiwa na Kiranja wa Wachache Peter Imwatok.

Mswada huo ambao notisi yake ilichapishwa wiki iliyopita na unaotazamiwa kuwasilishwa bungeni wiki hii, unapendekeza barabara ya Mbagathi Way ibadilishwe jina na kuitwa Raila Odinga Road.

Hatua hiyo ni kwa kutambua mchango wa waziri mkuu huyo wa zamani katika ukuaji wa nchi kutetea uongozi mzuri, kanuni za kidemokrasia na maendeleo ya miundomsingi.

You can share this post!

Wenye ardhi inayohusishwa na Ruto Laikipia hawajulikani

FKF yampa kocha mpya miezi 2 tu