Peru wakung’uta Paraguay na kutinga nusu-fainali za Copa America

Peru wakung’uta Paraguay na kutinga nusu-fainali za Copa America

Na MASHIRIKA

PERU waliwapepeta Paraguay 4-3 kupitia mikwaju ya penalti mnamo Ijumaa usiku na kufuzu kwa nusu-fainali za Copa America nchini Brazil.

Mshindi huo wa mechi hiyo aliamulia kupitia mikwaju ya penalti baada ya pande zote mbili kuambulia sare ya 3-3 kufikia mwisho wa muda wa ziada katika uwanja wa Olimpico mjini Goiania.

Gustavo Gomez wa Paraguay alionyeshwa kadi nyekundu mwishoni mwa kipindi cha kwanza kabla ya Andre Carrillo wa Peru pia kufurushwa uwanjani kwa kadi nyekundu mwishoni mwa kipindi cha pili.

Gomez aliwaweka Paraguay kifua mbele katika dakika ya 11 kabla ya kujifunga na kusawazishia Peru kunako dakika ya 21. Gianluca Lapadula aliwaweka Peru uongozini katika dakika ya 40 kabla ya juhudi zake kufutwa na Junior Alonso dakika 14 baadaye.

Ingawa Yoshimar Rotun alifungia Peru bao lililotazamiwa kuwa la ushindi katika dakika ya 80, fowadi Gabreil Avalos alisawazisha mambo na kuhakikisha kwamba mechi hiyo inaingia muda wa ziada.

Kipa Pedro Gallese wa Peru alipangua mkwaju wa

Alberto Espinola baada ya Miguel Trauco kufunga penalti yake kwa upande wa Peru. Daniel Martinez na Braian Samudio ndio wanasoka wengine waliopoteza penalti zao kwa upande wa Paraguay. Mikwaju ya Santiago Ormeno na Christian Cueva wa Peru ilipanguliwa na kipa Antony Silva wa Paraguay.

Peru sasa watavaana na Brazil kwenye nusu-fainali itakayochezewa katika uwanja wa Nilton Santos jijini Rio de Janeiro mnamo Julai 6, 2021. Watashuka dimbani wakilenga kuepuka makosa yaliyochangia kupigwa kwao na Brazil 4-0 kwenye hatua ya makundi.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Uingereza kigezoni wakijiandaa kuvaana na Ukraine kwenye...

EACC yagonga mwamba katika uchunguzi kuhusu vyeti feki vya...