Habari Mseto

Pesa zenu zi salama, KCB yawahakikishia wateja waliolalamika kupoteza maelfu kwa akaunti

March 14th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Benki ya KCB imejitetea kuhusiana na madai kuwa pesa za wateja wake zilikuwa zikipunguzwa bila wao kufahamishwa.

Machi 8, benki hiyo iliwahakikishia wateja wake kwamba pesa zao zilikuwa salama, licha ya malalamishi mengi katika mitandao ya kijamii.

Katika taarifa, benki hiyo ilisema kuwa pesa zote zilikuwa salama na kuongeza kuwa ilikuwa ikisuluhisha tatizo hilo ikiwa lilikuwa.

“Kama benki inayoaminika, tunachukulia suala la faragha ya wateja wetu kwa umuhimu mkubwa na kusuluhisha masuala yoyote yanayoweza kujitokeza kwa wateja wetu,” ilisema benki hiyo.

Baadhi ya wateja walilalamika kuwa walipoteza maelfu katika kisanga hicho.

Hata hivyo, benki hiyo iliomba kupewa muda kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na suala hilo.

Itawabidi wateja wake kungoja kwa mwezi mmoja kujua kilichofanyika.