Pigo Arsenal baada ya majeraha na corona kuweka nje mabeki tegemeo

Pigo Arsenal baada ya majeraha na corona kuweka nje mabeki tegemeo

Na MASHIRIKA

BEKI tegemeo kambini mwa Arsenal, Takehiro Tomiyasu sasa atakosa mechi kadhaa za klabu hiyo baada ya kupata jeraha wakati wa mchuano wa awali wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) uliowavunia ushindi wa 4-1 dhidi ya Leeds United ugani Elland Road.

Difenda huyo raia wa Japan hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachotegemewa na kocha Mikel Arteta dhidi ya Sunderland kwenye mchuano wa robo-fainali ya Carabao Cup mnamo Disemba 21, 2021. Arsenal pia itakosa huduma za beki Pablo Mari na kiungo Albert Sambi Lokonga wanaougua Covid-19.

Sunderland kwa upande wao wamefichua kwamba mchezaji mmoja alipatikana na virusi vya corona kutokana na vipimo vya Disemba 20, 2021 na atakosa mechi dhidi ya Arsenal ugani Emirates.

Sunderland watakosa pia maarifa ya mvamizi Leon Dajaku anayeuguza jeraha la mguu.

You can share this post!

FA yapiga Leeds United faini ya Sh3 milioni kwa utovu wa...

Wan-Bissaka atozwa faini na kupigwa marufuku ya kuendesha...

T L