Pigo kwa Arsenal baada ya Sheffield United kumkwamilia kipa Ramsdale

Pigo kwa Arsenal baada ya Sheffield United kumkwamilia kipa Ramsdale

Na MASHIRIKA

ARSENAL wamepata pigo baada ya kocha Slavisa Jokanovic wa Sheffield United kusisitiza kwamba hawana mpango wowote wa kumtia kipa Aaron Ramsdale, 23, mnadani.

Arsenal wamekuwa wakiwania huduma za kipa huyo raia wa Uingereza ili kumpiga jeki mlinda-lango wao chaguo la kwanza, Bernd Leno.

Ramsdale alihamia Sheffield United kutoka Bournemouth kwa kima cha Sh2.8 bilioni mnamo Juni 2020.

Kipa huyo aliitwa na kocha Gareth Southgate katika timu ya taifa ya Uingereza kwa ajili ya kipute cha Euro 2020 ila hakuwajibishwa katika mechi yoyote. Alipangwa katika kikosi cha kwanza cha Sheffield kwenye mchuano wa Ligi ya Daraja ya Kwanza (Championship) uliowashuhudia wakipigwa 1-0 na Birmingham mnamo Agosti 7, 2021.

Wakati uo huo, kiungo Joe Willock wa Arsenal ameafikiana na Newcastle United kwamba atajiunga nao kwa mkataba wa kudumu na tayari ametua uwanjani St James’ Park kufanyiwa vipimo vya afya.

Uhamisho wa Willock hadi Newcastle inayotiwa makali na kocha Steve Bruce unatarajiwa kugharimu Sh3.9 bilioni.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Cherargei akashifu Uhuru baada ya wanariadha waliowasili...

Kocha Marcelo Bielsa arefusha muda wa kuhudumu kwake Leeds...