Pigo kwa Everton fowadi tegemeo Dominic Calvert-Lewin akitarajiwa kusalia mkekani kwa wiki sita kuuguza jeraha la goti

Pigo kwa Everton fowadi tegemeo Dominic Calvert-Lewin akitarajiwa kusalia mkekani kwa wiki sita kuuguza jeraha la goti

Na MASHIRIKA

FOWADI mahiri wa Everton, Dominic Calvert-Lewin, 25, anatarajiwa kukosa mechi za wiki zita za ufunguzi wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo 2022-23 kutokana na jeraha la goti alilopata wakati wa mazoezi.

Nyota huyo raia wa Uingereza alisalia mkekani kwa miezi minne ya mwisho wa kampeni za msimu wa 2021-22 kwa sababu ya jeraha la misuli ya miguu.

Kuumia kwa Calvert-Lewin ni pigo kubwa kwa kocha Frank Lampard ambaye sasa atasalia bila fowadi tegemeo kikosini mwake baada ya mshambuliaji raia wa Brazil, Richarlson Andrade naye kuyoyomea kambini mwa Tottenham Hotspur kwa Sh8.6 bilioni.

Salomon Rondon, Demarai Gray, Alex Iwobi na Anthony Gordon sasa watakuwa washambuliaji tegemeo la Everton katika safu ya mbele hadi Calvert-Lewin atakapopona.

Everton wamepangiwa kufungua kampeni zao za EPL msimu wa 2022-23 dhidi ya Chelsea mnamo Agosti 6, 2022 uwanjani Goodison Park.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Kura: Machifu hawapigii debe Azimio – Kibicho

Biden hajapona corona, daktari wake asema

T L