Pigo kwa Liverpool baada ya kiungo Thiago Alcantara kupata jeraha la mguu

Pigo kwa Liverpool baada ya kiungo Thiago Alcantara kupata jeraha la mguu

Na MASHIRIKA

LIVERPOOL watakosa huduma za kiungo Thiago Alcantara katika michuano miwili ijayo kwa sababu ya jeraha la mguu.

Nyota mwenye umri wa miaka 30 aliumia alipokuwa akichezea waajiri wake katika mchuano wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) uliowapa ushindi wa 3-0 dhidi ya Crystal Palace mnamo Septemba 18, 2021.

Liverpool wamepangiwa kuvaana na Norwich City ugenini katika gozi la Carabao Cup mnamo Septemba 21, 2021 kabla ya kuwaendea limbukeni wa EPL Brentford mnamo Septemba 25, 2021.

“Siwezi kusema atakuwa nje kwa muda gani, lakini nijuavyo ni kwamba hatakuwa sehemu ya kikosi tutakachokitegemea dhidi ya Norwich au Brentford,” akasema kocha msaidizi wa Liverpool, Pep Lijnders.

Alcantara ambaye ni mchezaji wa zamani wa Bayern Munich, aliondolewa uwanjani katika dakika ya 62 na nafasi yake kutwaliwa na Naby Keita wakati wa mchuano wa EPL mnamo Septemba 18 ugani Anfield.

Beki Trent Alexander-Arnold ambaye alikosa mechi dhidi ya Palace pia hatawajibishwa dhidi ya Norwich. Kocha Jurgen Klopp atatumia kipute dhidi ya Norwich kumkaribisha kambini fowadi Roberto Firmino ambaye amerejelea mazoezi baada ya kukosa mechi tatu zilizopita za waajiri wake kutokana na jeraha la paja.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Mkenya Eric ‘Marcelo’ Ouma asaidia AIK kuongoza...

Keter, Munyes wakasirisha maseneta kwa kudinda kufika mbele...