Habari Mseto

Pigo kwa ODM kumpoteza Hatimy Mombasa

November 14th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Serikali ya Kaunti ya Mombasa inaomboleza kifo cha Diwani mteuliwa Mohammed Hatimy. Hatimy ambaye alikuwa mwenyekiti wa chama cha ODM Kaunti ya Mombasa alifariki kwa virusi vya corona.

Spika wa kaunti ya Mombasa Harub Khatri alisema kwamba Hatimy alifariki Jumamosi.

“Tulimpoteza asubuhi hii saa tisa usiku,”alisema spika.

Bw  Khatri alisema kwamba mwanasiasa huyo alikuwa kwenyee chumba cha watu maututi kwa wiki tatu.

Alikuwa kati ya madiwani ambao walipata virusi vya corona  na bunge likafungwa siku 14.

Chama ODM kilimwomboleza Hatiny kuwa kiongozi huyo kuwa mwanamume dhabiti.

“Familia ya ODM imepoteza mwanamume mzuri na kiongozi. Mheshimiwa Mohamed Hatimy Kuanti mwenyekiti wa Kaunti ya Mombasa na Diwani aliyekuwa anafanya kazi kwa muhula wa pili amefariki,ilisema ODM  kwenye mtandao wa Twitter.