Pigo kwa Spurs fowadi Kane akiumia katika sare ya 2-2 dhidi ya Everton ligini

Pigo kwa Spurs fowadi Kane akiumia katika sare ya 2-2 dhidi ya Everton ligini

Na MASHIRIKA

MSHAMBULIAJI Harry Kane alipachika wavuni mabao mawili na kufuta juhudi za kiungo Gylfi Sigurdsson aliyefungia pia waajiri wake Everton magoli mawili kwenye sare ya 2-2 waliyoisajili dhidi ya Tottenham Hotspur katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Ijumaa usiku.

Kane ambaye ni raia wa Uingereza alichuma nafuu kutokana na masihara ya mabeki wa Everton na kuwaweka Spurs kifua mbele katika dakika ya 27 kabla ya kusawazisha mambo kunako dakika ya 68.

Awali, Sigurdsson alikuwa amewasawazishia Everton kupitia penalti ya dakika ya 31 kabla ya kuwaweka waajiri wake kifua mbele kunako dakika ya 62.

Bao lake la pili lilikuwa zao la ushirikiano mkubwa kati yake na kiungo Seamus Coleman.

Zaidi ya sare, pigo kubwa zaidi kwa Spurs ni jeraha la lililomweka Kane katika ulazima wa kuondolewa uwanjani mwishoni mwa kipindi cha pili.

Everton wangalifunga bao la ushindi sekunde chache kabla ya kutamatika kwa kipindi cha pili ila kipa Hugo Lloris akapangua makombora mazito aliyoelekezewa kupitia Joshua King pamoja na Richarlison Andrade.

Matokeo ya mechi hiyo yalisaza Spurs katika nafasi ya saba jedwalini kwa alama 50, tano nyuma ya West Ham United wanaofunga orodha ya nne-bora. Everton ya kocha Carlo Ancelotti inashikilia nafasi ya nane kwa pointi 49.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Mjakazi kupimwa akili

Hali mbaya ya uchumi yatia hofu Wakenya wengi –...