Michezo

‘Pique nifunge bao upesi Miss Bumbum akukome’

April 15th, 2019 2 min read

Na CHRIS ADUNGIO

MWANAMUZIKI mzaliwa wa Colombia, Shakira Isabel ambaye ni mkewe Gerrard Pique amemtaka mumewe kukatiza kabisa mawasiliano yote na mwanamitindo Suzy Cortez ambaye ameanza kumtambalia upya beki huyo wa Barcelona.

Isitoshe, kipusa huyo amemtaka mumewe amfunge bao la tatu la kimapenzi litakalohesabiwa rasmi na refa wa mahaba wakati akiadhimisha miaka 43 ya kuzaliwa kwake mnamo Februari mwakani.

Kulingana na gazeti la The Sun, Shakira, 42, anahisi kwamba mumewe mwenye umri wa miaka 32 huenda akashawishika kutoka kimapenzi na Suzy, mshindi wa zamani wa taji la Miss BumBum.

Suzy aliye na umri wa miaka 28, amekuwa na mazoea ya kuvua nguo na kusalia uchi wa mnyama kila mara Pique anapowatambisha waajiri wake uwanjani Camp Nou.

“Shakira na Antonella sasa wamo katika kapu moja. Vipusa hawa hawalali wakiwazia mbinu za kumzuia Suzy kuyafikia madume yao!”

Mnamo Septemba 2017, Antonella ambaye ni mkewe Lionel Messi, alimshinikiza fowadi huyo kutia chale zenye michoro ya midomo yake (Antonella) pajani ili iwe ishara ya kiwango cha ukomavu wa penzi lao!

Pindi alipochora ‘midomo’ ya mkewe katika sehemu za paja lake la kushoto, ilimjuzu Messi kutuma picha kwenye mtandao wake wa Instagram ili kuiridhisha nafsi ya mkewe ambaye kwa sasa ametishia kumtema iwapo mvamizi huyo ataendelea kumruhusu Suzy kumtia kishawishini.

Sawa na Antonella, ambacho kwa sasa kinamkoroga nyongo Shakira ni hatua ya Pique kuanza kuwasiliana na Suzy mitandaoni huku wakibadilishana video na picha za kila sampuli.

Karibuni, Suzy amekuwa mwepesi wa kupakia tena picha zake za uchi mitandaoni kisha kumtumia Pique kupitia Instagram huku akimshawishi kufanya hima alitikise buyu lake la asali.

“Pique, achana na mwendo wa kobe katika hili suala la penzi. Njoo upesi ulimenye tunda,” akaandika Suzy katika miongoni mwa jumbe zake mitandaoni.

Kwa pamoja, wawili hao wamejaliwa watoto wawili: Milan, 6, na Sasha, 4. Kabla ya kuanza kutoka kimapenzi na Shakira mnamo 2010, Pique alikuwa akijirinia asali katika mizinga ya vidosho Nuria Tomas na Lisa Lazarus.

Hatua ya Suzy kutafuta upya hifadhi ya penzi lake kwa Pique inajiri miezi kadhaa baada ya kipusa huyo kupuu- zwa na Neymar Jr, Philippe Coutinho na Messi. Suzy

alitawazwa mshindi wa Miss BumBum mnamo 2015 kutokana na ukubwa wa makalio yake.