Habari Mseto

Polisi 6 walazwa baada ya kupigwa na umma

August 16th, 2020 1 min read

MARY WAMBUI na FAUSTINE NGILA

Polisi sita wanauguza majeraha baada ya kushambuliwa na umma uliokuwa na ngadhabu huku wakiandamana kutokana na kifo cha watu wanne kutokana na ajali iliyotokea Kakamega Kaskazini Jumamosi.

Kolplo Barnabas Koech,Elnathan Bett na Alloyce Nzuki na Konstebo Lawrence Omondi ,Dancun Onyango na Erick Anari waliumizwa kichwa ,miguu na kifua walipokuwa wakijaribu kutuliza umati huo wa watu waliwapiga mawe.

Walitibiwa hospitali ya kaunti ndogo ya Malava na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Ajali hio ya Jumamosi ilitokea baada ya dereva wa kampuni ya Sukari West Kenya kukosa mwelekeo na kugoga mtu wa pikipiki na kusambabishwa vifo vya watu wanne.

Malori matatu yalichomwa na mengine 12 kuharibiwa huku ikiwalazimu polisi kupiga risasi hewani.