Habari Mseto

Polisi afariki hospitalini baada ya kujipiga risasi

October 29th, 2020 1 min read

Dickens Wasonga na Faustine Ngila

Afisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Madundu Kaunti ya Siaya alifariki alipokuwa akipokea matibabu Jumatatu asubuhi kwenye hospitali ya rufaa ya Siaya.

Kamanda wa polisi Kaunti ndogo ya Ugunja Bw Lazarus Tarus alisema kwamba afisa huyo alifariki kutokana majeraha alipokuwa akitibiwa baada ya kujipiga risasi Jumatatu asubuhi.

Maafisa wezake walisema kwamba walipata mwezao akiwa na anavunja dam una wakamkibiza hospitali ya Ambira kufuatia kisa hicho cha asubuhi.

Baadaye alihamishwa kwenye hospitali ya rufaa ya Siaya lakini akafariki kutokana na majerha aliyopata.

Ripoti za polisi zilizoneekana na Taifa Leo zilisema kwamba afisa huyo alikuwa amepewa bunduki aina ya G3 na kupewa kazi kwenye kituo hicho.

Mlio wa risasi ulisikika nyumbani kwake ambaye ikokaribu na afasi ya kuandikisha taarifa.