Habari Mseto

Polisi afariki kwenye ajali Karura

October 20th, 2020 1 min read

NA MACHARIA MWANGI

Afisa wa polisi alifariki  baada ya pikipiki aliyokuwa akiendesha kugongana na matatu eneo la Karura, barabara ya Naivasha kuelekea Gilgil..

Kulingana na kamanda wa polisi wa Gilgil Bw Henry Mbogo afisa huyo alipata maumivu kichwani na kufariki alipofikishwa hospitali ya St Mary’s.

Bw Mbogo alisema kwamba matatu hiyo ilikuwa inaeleka upande wa Nakuru na polisi huyo alikuwa anatoka upande huo Jumatatu asubuhi wakati ajali hiyo ilipotokea..

“Matatu hiyo ilikuwa inajaribu kupita lori wakati iligogana na pikipiki hiyo na trela,” alisema Bw Mbogo..

Aliogeza kwamba afisa wa polisi mwingine aliyekuwa karibu naye alipata majeraha kiasi. Bw Mbogo alisema kwamba abiria wa matatu hiyo hawakuumia.

Matatu hiyo ilipelekwa kituo cha polisi cha Giligil huku uchunguzi ukiendelea kufanyika. Tukio hilo lilijiri siku moja baada ya watu watano kupoteza maisha yao eneo la Laini Naivasha -Gilgil Jumapili jioni..

Watu watatu walifariki papo kwa hapo huku wawili wakifariki walipokuwa wakipokea matibabu kwenye hospitali ya Naivasha.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA