Habari Mseto

Polisi aliyeuawa Nyahururu azikwa

November 10th, 2020 1 min read

NA WAIKWA MAINA

Afisa wa polisi wa kituo cha polisi cha Nyahururu aliyeuwawa na watu wasiojulikana alizikwa Ijumaa asubuhi. Wakati wa Mazishi yake, David Murai Spika wa bunge la Nyandarua aliomba DCI kufanya uchunguzi na kukamata wauaji hao.

Baada ya upasuaji kufanywa ulionyesha kwamba afisa huyo alipewaa sum una baada ye akanyongwa hadi kifo.

Ripoti zilionyesha kwamba waliomuua afisa huyo walimkanyangga kifuani mara kadhaa kabla ya kufariki.Maafisa walisema kwamba afisa huyo labda aliuliwa kwingine kabla ya kuletwa nyumbani kwake mtaa wa Garden Estate Nyahururu ambapo alipatikana.

Maafisa wezake wakiogozwa na afisa wa Titus Etiang walimtaja afisa huyo kuwa mwenye bidii na ajiyetolea kazini.

Bw  Samuel Murai, dunguye wa afisa aliyeuliwa aliomba uchunguzi ufanyike kwa haraka.

Tunataka haki kwa dunguyetu muuaji lazima akamatwe .Tutaeleza aje kifo chake kwa wtoto wake .Hakufaa kukufa kifo cha ungungu,”alisema dunguye Bw Murai.

Naibu Kamanda wa polisi wa Nyahururu  Moffat Mong’era alisema kwamba mwanaamke mmoja likamatwa kufuatia kifo cha  afisa huyo.

“Ni bahati mbaya kupoteza afisa kkama huyo kwenye mazingira yasioeleweka.Uchunguzi unaendelea kubaini kilichisababisha kifo hicho na waliosababisha mauaji hayo,”alisema mkuu wa polisi.